• 1. Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu,

  • 2. Mfalme wa wanaadamu,

  • 3. Mungu wa wanaadamu,

  • 4. Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas,

  • 5. Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu,

  • 6. Kutokana na majini na wanaadamu.