logo HARUN YAHYA

Al-A`la - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,
  • 2. Aliye umba, na akaweka sawa,
  • 3. Na ambaye amekadiria na akaongoa,
  • 4. Na aliye otesha malisho,
  • 5. Kisha akayafanya makavu, meusi.
  • 6. Tutakusomesha wala hutasahau,
  • 7. Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.
  • 8. Na tutakusahilishia yawe mepesi.
  • 9. Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
  • 10. Atakumbuka mwenye kuogopa.
  • 11. Na atajitenga mbali nayo mpotovu,
  • 12. Ambaye atauingia Moto mkubwa.
  • 13. Tena humo hatakufa wala hawi hai.
  • 14. Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.
  • 15. Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.
  • 16. Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!
  • 17. Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
  • 18. Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,
  • 19. Vitabu vya Ibrahimu na Musa.
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code