logo HARUN YAHYA

At-Tin - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Naapa kwa tini na zaituni!
  • 2. Na kwa Mlima wa Sinai!
  • 3. Na kwa mji huu wenye amani!
  • 4. Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.
  • 5. Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!
  • 6. Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha.
  • 7. Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?
  • 8. Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code