logo HARUN YAHYA

Al-`Alaq - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,
  • 2. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,
  • 3. Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
  • 4. Ambaye amefundisha kwa kalamu.
  • 5. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
  • 6. Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri
  • 7. Akijiona katajirika.
  • 8. Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.
  • 9. Umemwona yule anaye mkataza
  • 10. Mja anapo sali?
  • 11. Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu?
  • 12. Au anaamrisha uchamngu?
  • 13. Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?
  • 14. Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?
  • 15. Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!
  • 16. Shungi la uwongo, lenye makosa!
  • 17. Basi na awaite wenzake!
  • 18. Nasi tutawaita Mazabania!
  • 19. Hasha! Usimt`ii! Nawe sujudu na ujongee!
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code