logo HARUN YAHYA

Al-Inshiqaq - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Itapo chanika mbingu,
  • 2. Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
  • 3. Na ardhi itakapo tanuliwa,
  • 4. Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu,
  • 5. Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
  • 6. Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.
  • 7. Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia,
  • 8. Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi,
  • 9. Na arudi kwa ahali zake na furaha.
  • 10. Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,
  • 11. Basi huyo ataomba kuteketea.
  • 12. Na ataingia Motoni.
  • 13. Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.
  • 14. Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.
  • 15. Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!
  • 16. Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,
  • 17. Na kwa usiku na unavyo vikusanya,
  • 18. Na kwa mwezi unapo pevuka,
  • 19. Lazima mtapanda t`abaka kwa t`abaka!
  • 20. Basi wana nini hawaamini?
  • 21. Na wanapo somewa Qur`ani hawasujudu?
  • 22. Bali walio kufuru wanakanusha tu.
  • 23. Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria.
  • 24. Basi wabashirie adhabu chungu!
  • 25. Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika.
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code