Nuh - QURAN - Harun Yahya
-
1. Hakika Sisi tulimtuma Nuh`u kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu.
-
2. Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhaahiri kwenu,
-
3. Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumt`ii.
-
4. Atakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda ulio wekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua!
-
5. Akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana,
-
6. Lakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia.
-
7. Na hakika mimi kila nilipo waita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno!
-
8. Tena niliwaita kwa uwazi,
-
9. Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri.
-
10. Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe.
-
11. Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo.
-
12. Na atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito.
-
13. Mna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu?
-
14. Na hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja?
-
15. Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka?
-
16. Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa?
-
17. Na Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi kama mimea.
-
18. Kisha atakurudsheni humo na atakutoeni tena.
-
19. Na Mwenyezi Mungu amekukunjulieni ardhi kama busati.
-
20. Ili mtembee humo katika njia zilizo pana.
-
21. Nuh`u akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila khasara.
-
22. Na wakapanga vitimbi vikubwa.
-
23. Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa` wala Yaghutha, wala Yau`qa, wala Nasra.
-
24. Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.
-
25. Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu.
-
26. Na Nuh`u akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri!
-
27. Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.
-
28. Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.
SHIRIKI
1
Al-Fatihah
2
Al Baqara
3
Ali `Imran
4
An-Nisa
5
Al-Ma`idah
6
Al-An`am
7
Al-A`raf
8
Al-Anfal
9
At-Tawbah
10
Yunus
11
Hud
12
Yusuf
13
Ar-Ra`d
14
Ibrahim
15
Al-Hijr
16
An-Nahl
17
Al-Isra
18
Al-Kahf
19
Maryam
20
Taha
21
Al-Anbya
22
Al-Haj
23
Al-Mu`minun
24
An-Nur
25
Al-Furqan
26
Ash-Shu`ara
27
An-Naml
28
Al-Qasas
29
Al-`Ankabut
30
Ar-Rum
31
Luqman
32
As-Sajdah
33
Al-Ahzab
34
Saba
35
Faatir
36
Ya-Sin
37
As-Saffat
38
Sad
39
Az-Zumar
40
Ghafir
41
Fussilat
42
sh-Shuraa
43
Az-Zukhruf
44
Ad-Dukhan
45
Al-Jathiyah
46
Al-Ahqaf
47
Muhammad
48
Al-Fath
49
Al-Hujurat
50
Qaf
51
Adh-Dhariyat
52
At-Tur
53
An-Najm
54
Al-Qamar
55
Ar-Rahman
56
Al-Waqi`ah
57
Al-Hadid
58
Al-Mujadila
59
Al-Hashr
60
Al-Mumtahanah
61
As-Saf
62
Al-Jumu`ah
63
Al-Munafiqun
64
At-Taghabun
65
At-Talaq
66
At-Tahrim
67
Al-Mulk
68
Al-Qalam
69
Al-Haqqah
70
Al-Ma`arij
71
Nuh
72
Al-Jinn
73
Al-Muzzammil
74
Al-Muddaththir
75
Al-Qiyamah
76
Al-Insan
77
Al-Mursalat
78
An-Naba
79
An-Nazi`at
80
Abasa
81
At-Takwir
82
Al-Infitar
83
Al-Mutaffifin
84
Al-Inshiqaq
85
Al-Buruj
86
At-Tariq
87
Al-A`la
88
Al-Ghashiyah
89
Al-Fajr
90
Al-Balad
91
Ash-Shams
92
Al-Layl
93
Ad-Duhaa
94
Ash-Sharh
95
At-Tin
96
Al-`Alaq
97
Al-Qadr
98
Al-Bayyinah
99
Az-Zalzalah
100
Al-`Adiyat
101
Al-Qari`ah
102
At-Takathur
103
Al-`Asr
104
Al-Humazah
105
Al-Fil
106
Quraysh
107
Al-Ma`un
108
Al-Kawthar
109
Al-Kafirun
110
An-Nasr
111
Al-Masad
112
Al-Ikhlas
113
Al-Falaq
114
An-Nas