• 1. Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!

  • 2. Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!

  • 3. Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?

  • 4. Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!

  • 5. Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake.

  • 6. Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?

  • 7. Basi jicho litapo dawaa,

  • 8. Na mwezi utapo patwa,

  • 9. Na likakusanywa jua na mwezi,

  • 10. Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?

  • 11. La! Hapana pa kukimbilia!

  • 12. Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.

  • 13. Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha.

  • 14. Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.

  • 15. Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.

  • 16. Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.

  • 17. Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.

  • 18. Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.

  • 19. Kisha ni juu yetu kuubainisha.

  • 20. Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,

  • 21. Na mnaacha maisha ya Akhera.

  • 22. Zipo nyuso siku hiyo zitao ng`ara,

  • 23. Zinamwangallia Mola wao Mlezi.

  • 24. Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana.

  • 25. Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.

  • 26. La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo,

  • 27. Na pakasemwa: Nani wa kumganga?

  • 28. Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki;

  • 29. Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi,

  • 30. Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!

  • 31. Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali.

  • 32. Bali alikanusha, na akageuka.

  • 33. Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao.

  • 34. Ole wako, ole wako!

  • 35. Kisha Ole wako, ole wako!

  • 36. Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?

  • 37. Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?

  • 38. Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.

  • 39. Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.

  • 40. Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?