Al-Qamar - QURAN - Harun Yahya
-
1. Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!
-
2. Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.
-
3. Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti.
-
4. Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio.
-
5. Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu!
-
6. Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha;
-
7. Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika,
-
8. Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu.
-
9. Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa.
-
10. Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru!
-
11. Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika.
-
12. Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa.
-
13. Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba.
-
14. Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa.
-
15. Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye kumbuka?
-
16. Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu.
-
17. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur`ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka?
-
18. Kina A`di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
-
19. Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo,
-
20. Ukiwang`oa watu kama vigogo vya mitende vilio ng`olewa.
-
21. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
-
22. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur`ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anaye kumbuka?
-
23. Thamudi waliwakanusha Waonyaji.
-
24. Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa!
-
25. Ni yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi!
-
26. Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi.
-
27. Hakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame tu na ustahamili.
-
28. Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliye khusika.
-
29. Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja.
-
30. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu!
-
31. Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea uwa.
-
32. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur`ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye?
-
33. Kaumu Lut`i nao waliwakadhibisha Waonyaji.
-
34. Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa wafuasi wa Lut`i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri.
-
35. Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye shukuru.
-
36. Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo.
-
37. Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu!
-
38. Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea.
-
39. Basi onjeni adhabu na maonyo yangu!
-
40. Na hakika tumeisahilisha Qur`ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka?
-
41. Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni.
-
42. Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo shika Mwenye nguvu Mwenye uweza.
-
43. Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani?
-
44. Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu.
-
45. Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma.
-
46. Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi.
-
47. Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu.
-
48. Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu!
-
49. Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.
-
50. Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.
-
51. Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka?
-
52. Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni.
-
53. Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa.
-
54. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito.
-
55. Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.
SHIRIKI
1
Al-Fatihah
2
Al Baqara
3
Ali `Imran
4
An-Nisa
5
Al-Ma`idah
6
Al-An`am
7
Al-A`raf
8
Al-Anfal
9
At-Tawbah
10
Yunus
11
Hud
12
Yusuf
13
Ar-Ra`d
14
Ibrahim
15
Al-Hijr
16
An-Nahl
17
Al-Isra
18
Al-Kahf
19
Maryam
20
Taha
21
Al-Anbya
22
Al-Haj
23
Al-Mu`minun
24
An-Nur
25
Al-Furqan
26
Ash-Shu`ara
27
An-Naml
28
Al-Qasas
29
Al-`Ankabut
30
Ar-Rum
31
Luqman
32
As-Sajdah
33
Al-Ahzab
34
Saba
35
Faatir
36
Ya-Sin
37
As-Saffat
38
Sad
39
Az-Zumar
40
Ghafir
41
Fussilat
42
sh-Shuraa
43
Az-Zukhruf
44
Ad-Dukhan
45
Al-Jathiyah
46
Al-Ahqaf
47
Muhammad
48
Al-Fath
49
Al-Hujurat
50
Qaf
51
Adh-Dhariyat
52
At-Tur
53
An-Najm
54
Al-Qamar
55
Ar-Rahman
56
Al-Waqi`ah
57
Al-Hadid
58
Al-Mujadila
59
Al-Hashr
60
Al-Mumtahanah
61
As-Saf
62
Al-Jumu`ah
63
Al-Munafiqun
64
At-Taghabun
65
At-Talaq
66
At-Tahrim
67
Al-Mulk
68
Al-Qalam
69
Al-Haqqah
70
Al-Ma`arij
71
Nuh
72
Al-Jinn
73
Al-Muzzammil
74
Al-Muddaththir
75
Al-Qiyamah
76
Al-Insan
77
Al-Mursalat
78
An-Naba
79
An-Nazi`at
80
Abasa
81
At-Takwir
82
Al-Infitar
83
Al-Mutaffifin
84
Al-Inshiqaq
85
Al-Buruj
86
At-Tariq
87
Al-A`la
88
Al-Ghashiyah
89
Al-Fajr
90
Al-Balad
91
Ash-Shams
92
Al-Layl
93
Ad-Duhaa
94
Ash-Sharh
95
At-Tin
96
Al-`Alaq
97
Al-Qadr
98
Al-Bayyinah
99
Az-Zalzalah
100
Al-`Adiyat
101
Al-Qari`ah
102
At-Takathur
103
Al-`Asr
104
Al-Humazah
105
Al-Fil
106
Quraysh
107
Al-Ma`un
108
Al-Kawthar
109
Al-Kafirun
110
An-Nasr
111
Al-Masad
112
Al-Ikhlas
113
Al-Falaq
114
An-Nas