logo HARUN YAHYA

Ad-Duhaa - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Naapa kwa mchana!
  • 2. Na kwa usiku unapo tanda!
  • 3. Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
  • 4. Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
  • 5. Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
  • 6. Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
  • 7. Na akakukuta umepotea akakuongoa?
  • 8. Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
  • 9. Basi yatima usimwonee!
  • 10. Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!
  • 11. Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code