logo HARUN YAHYA

At-Tariq - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!
  • 2. Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?
  • 3. Ni Nyota yenye mwanga mkali.
  • 4. Hapana nafsi ila inayo mwangalizi.
  • 5. Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?
  • 6. Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,
  • 7. Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.
  • 8. Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.
  • 9. Siku zitakapo dhihirishwa siri.
  • 10. Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.
  • 11. Naapa kwa mbingu yenye marejeo!
  • 12. Na kwa ardhi inayo pasuka!
  • 13. Hakika hii ni kauli ya kupambanua.
  • 14. Wala si mzaha.
  • 15. Hakika wao wanapanga mpango.
  • 16. Na Mimi napanga mpango.
  • 17. Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code