logo HARUN YAHYA

Al-Ghashiyah - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?
  • 2. Siku hiyo nyuso zitainama,
  • 3. Zikifanya kazi, nazo taabani.
  • 4. Ziingie katika Moto unao waka -
  • 5. Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.
  • 6. Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.
  • 7. Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.
  • 8. Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.
  • 9. Zitakuwa radhi kwa juhudi yao,
  • 10. Katika Bustani ya juu.
  • 11. Hawatasikia humo upuuzi.
  • 12. Humo imo chemchem inayo miminika.
  • 13. Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,
  • 14. Na bilauri zilizo pangwa,
  • 15. Na matakia safu safu,
  • 16. Na mazulia yaliyo tandikwa.
  • 17. Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
  • 18. Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?
  • 19. Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?
  • 20. Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?
  • 21. Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
  • 22. Wewe si mwenye kuwatawalia.
  • 23. Lakini anaye rudi nyuma na kukataa,
  • 24. Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!
  • 25. Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
  • 26. Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code