logo HARUN YAHYA

Abasa - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Alikunja kipaji na akageuka,
  • 2. Kwa sababu alimjia kipofu!
  • 3. Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
  • 4. Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?
  • 5. Ama ajionaye hana haja,
  • 6. Wewe ndio unamshughulikia?
  • 7. Na si juu yako kama hakutakasika.
  • 8. Ama anaye kujia kwa juhudi,
  • 9. Naye anaogopa,
  • 10. Ndio wewe unampuuza?
  • 11. Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
  • 12. Basi anaye penda akumbuke.
  • 13. Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,
  • 14. Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.
  • 15. Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,
  • 16. Watukufu, wema.
  • 17. Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?
  • 18. Kwa kitu gani amemuumba?
  • 19. Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.
  • 20. Kisha akamsahilishia njia.
  • 21. Kisha akamfisha, akamtia kaburini.
  • 22. Kisha apendapo atamfufua.
  • 23. La! Hajamaliza aliyo muamuru.
  • 24. Hebu mtu na atazame chakula chake.
  • 25. Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
  • 26. Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
  • 27. Kisha tukaotesha humo nafaka,
  • 28. Na zabibu, na mimea ya majani,
  • 29. Na mizaituni, na mitende,
  • 30. Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
  • 31. Na matunda, na malisho ya wanyama;
  • 32. Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
  • 33. Basi utakapo kuja ukelele,
  • 34. Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,
  • 35. Na mamaye na babaye,
  • 36. Na mkewe na wanawe -
  • 37. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.
  • 38. Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,
  • 39. Zitacheka, zitachangamka;
  • 40. Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
  • 41. Giza totoro litazifunika,
  • 42. Hao ndio makafiri watenda maovu.
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code