logo HARUN YAHYA

Al-Layl - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Naapa kwa usiku unapo funika!
  • 2. Na mchana unapo dhihiri!
  • 3. Na kwa Aliye umba dume na jike!
  • 4. Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.
  • 5. Ama mwenye kutoa na akamchamngu,
  • 6. Na akaliwafiki lilio jema,
  • 7. Tutamsahilishia yawe mepesi.
  • 8. Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake,
  • 9. Na akakanusha lilio jema,
  • 10. Tutamsahilishia yawe mazito!
  • 11. Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia?
  • 12. Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu.
  • 13. Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
  • 14. Basi nakuonyeni na Moto unao waka!
  • 15. Hatauingia ila mwovu kabisa!
  • 16. Anaye kadhibisha na kupa mgongo.
  • 17. Na mchamngu ataepushwa nao,
  • 18. Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
  • 19. Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.
  • 20. Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
  • 21. Naye atakuja ridhika!
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code