logo HARUN YAHYA

Al-Infitar - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Mbingu itapo chanika,
  • 2. Na nyota zitapo tawanyika,
  • 3. Na bahari zitakapo pasuliwa,
  • 4. Na makaburi yatapo fukuliwa,
  • 5. Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma.
  • 6. Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?
  • 7. Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha,
  • 8. Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga.
  • 9. Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo.
  • 10. Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu,
  • 11. Waandishi wenye hishima,
  • 12. Wanayajua mnayo yatenda.
  • 13. Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema,
  • 14. Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni;
  • 15. Wataingia humo Siku ya Malipo.
  • 16. Na hawatoacha kuwamo humo.
  • 17. Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
  • 18. Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
  • 19. Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code