logo HARUN YAHYA

Al-`Adiyat - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
  • 2. Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
  • 3. Wakishambulia wakati wa asubuhi,
  • 4. Huku wakitimua vumbi,
  • 5. Na wakijitoma kati ya kundi,
  • 6. Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
  • 7. Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
  • 8. Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
  • 9. Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
  • 10. Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
  • 11. Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code