logo HARUN YAHYA

Ash-Shams - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Naapa kwa jua na mwangaza wake!
  • 2. Na kwa mwezi unapo lifuatia!
  • 3. Na kwa mchana unapo lidhihirisha!
  • 4. Na kwa usiku unapo lifunika!
  • 5. Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga!
  • 6. Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza!
  • 7. Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza!
  • 8. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake,
  • 9. Hakika amefanikiwa aliye itakasa,
  • 10. Na hakika amekhasiri aliye iviza.
  • 11. Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao,
  • 12. Alipo simama mwovu wao mkubwa,
  • 13. Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.
  • 14. Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.
  • 15. Wala Yeye haogopi matokeo yake.
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code