logo HARUN YAHYA

At-Tur - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Naapa kwa mlima wa T`ur,
  • 2. Na Kitabu kilicho andikwa
  • 3. Katika ngozi iliyo kunjuliwa,
  • 4. Na kwa Nyumba iliyo jengwa,
  • 5. Na kwa dari iliyo nyanyuliwa,
  • 6. Na kwa bahari iliyo jazwa,
  • 7. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea.
  • 8. Hapana wa kuizuia.
  • 9. Siku zitakapo tikisika mbingu kwa mtikiso,
  • 10. Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa.
  • 11. Basi ole wao siku hiyo hao wanao kadhibisha,
  • 12. Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi.
  • 13. Siku watapo sukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu,
  • 14. (Waambiwe): Huu ndio ule Moto mlio kuwa mkiukanusha!
  • 15. Je! Huu ni uchawi, au hamwoni tu?
  • 16. Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyo kuwa mkiyatenda.
  • 17. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na neema,
  • 18. Wakifurahi kwa yale aliyo wapa Mola wao Mlezi. Na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni.
  • 19. Kuleni na kunyweni kwa raha kabisa kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyatenda.
  • 20. Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza mahuru-l-aini.
  • 21. Na walio amini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima atapata alicho kichuma.
  • 22. Na tutawapa matunda, na nyama kama watavyo penda.
  • 23. Watapeana humo bilauri zisio na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi.
  • 24. Iwe wanawapitia watumishi wao kama kwamba ni lulu zilizomo katika chaza.
  • 25. Wataelekeana wakiulizana.
  • 26. Waseme: Tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa;
  • 27. Basi Mwenyezi Mungu akatufanyia hisani na akatulinda na adhabu ya upepo wa Moto.
  • 28. Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwenye kurehemu.
  • 29. Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu.
  • 30. Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari.
  • 31. Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia.
  • 32. Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu?
  • 33. Au ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini!
  • 34. Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli.
  • 35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?
  • 36. Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini.
  • 37. Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka?
  • 38. Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi!
  • 39. Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana?
  • 40. Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama?
  • 41. Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wameandika?
  • 42. Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao walio kufuru ndio watakao tegeka.
  • 43. Au wanae mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Subhanallah! Ametaksika Mwenyezi Mungu na hao wanao washirikisha naye.
  • 44. Na hata wange ona pande linatoka mbinguni linaanguka wange sema: Ni mawingu yaliyo bebana.
  • 45. Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapo hilikishwa.
  • 46. Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa.
  • 47. Na hakika walio dhulumu watapata adhabu nyengine isiyo kuwa hii, lakini wengi wao hawajui.
  • 48. Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo simama,
  • 49. Na usiku pia mtakase, na zinapo kuchwa nyota.
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code