105. Al-Fil - Qurani
- 1. Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?
- 2. Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?
- 3. Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi,
- 4. Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni,
- 5. Akawafanya kama majani yaliyo liwa!