• 1. Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo?

  • 2. Huyo ndiye anaye msukuma yatima,

  • 3. Wala hahimizi kumlisha masikini.

  • 4. Basi, ole wao wanao sali,

  • 5. Ambao wanapuuza Sala zao;

  • 6. Ambao wanajionyesha,

  • 7. Nao huku wanazuia msaada.