logo HARUN YAHYA

Al-Balad - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Naapa kwa Mji huu!
  • 2. Nawe unaukaa Mji huu.
  • 3. Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa.
  • 4. Hakika tumemuumba mtu katika taabu.
  • 5. Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?
  • 6. Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.
  • 7. Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?
  • 8. Kwani hatukumpa macho mawili?
  • 9. Na ulimi, na midomo miwili?
  • 10. Na tukambainishia zote njia mbili?
  • 11. Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.
  • 12. Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?
  • 13. Kumkomboa mtumwa;
  • 14. Au kumlisha siku ya njaa
  • 15. Yatima aliye jamaa,
  • 16. Au masikini aliye vumbini.
  • 17. Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.
  • 18. Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.
  • 19. Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.
  • 20. Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code