logo HARUN YAHYA

Al-Mursalat - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!
  • 2. Na zinazo vuma kwa kasi!
  • 3. Na zikaeneza maeneo yote!
  • 4. Na zinazo farikisha zikatawanya!
  • 5. Na zinazo peleka mawaidha!
  • 6. Kwa kuudhuru au kuonya,
  • 7. Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa!
  • 8. Wakati nyota zitakapo futwa,
  • 9. Na mbingu zitakapo pasuliwa,
  • 10. Na milima itakapo peperushwa,
  • 11. Na Mitume watakapo wekewa wakati wao,
  • 12. Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?
  • 13. Kwa siku ya kupambanua!
  • 14. Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini?
  • 15. Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha!
  • 16. Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia?
  • 17. Kisha tukawafuatilizia walio fuatia?
  • 18. Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!
  • 19. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
  • 20. Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
  • 21. Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
  • 22. Mpaka muda maalumu?
  • 23. Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
  • 24. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
  • 25. Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
  • 26. Walio hai na maiti?
  • 27. Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?
  • 28. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
  • 29. Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
  • 30. Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
  • 31. Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
  • 32. Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!
  • 33. Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!
  • 34. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
  • 35. Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
  • 36. Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
  • 37. Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
  • 38. Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia.
  • 39. Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
  • 40. Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
  • 41. Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,
  • 42. Na matunda wanayo yapenda,
  • 43. Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.
  • 44. Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema.
  • 45. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
  • 46. Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
  • 47. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
  • 48. Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
  • 49. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
  • 50. Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code