logo HARUN YAHYA

Al-Qari`ah - QURAN - Harun Yahya

  • 1. Inayo gonga!
  • 2. Nini Inayo gonga?
  • 3. Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?
  • 4. Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;
  • 5. Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!
  • 6. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
  • 7. Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
  • 8. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
  • 9. Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
  • 10. Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?
  • 11. Ni Moto mkali!
SHIRIKI
Facebook
X
WhatsApp
Telegram
QR Code
QR Code